Tag: Tanzania

WAWILI KUIWAKILISHA TANZANIA KWENYE MASHINDANO YA KUHIFADHI QURAN

Mstahiki Meya  wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Chaulembo (kushoto) akikabidhi bendera ya Taifa ili kuiwakilisha nchi katika mashindano  ya 19 ya kusoma na kuhifadhi Quran tukufu Afrika.

Watanzania wawili wamekabidhiwa bendera ya Taifa ili kuiwakilisha nchi katika mashindano makubwa ya 19 ya kusoma na kuhifadhi Quran tukufu Afrika yatakayofanyika nchini.

Akikabidhi bendera hiyo Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Chaulembo, kwa wawakilishi pekee ambao ni Shujaa Sulemani kutoka Morogoro na Mbwana Dadi kutoka Pemba amesema kuwa, imezoeleka mara nyingi bendera yetu wanakabidhiwa timu za mpira, lakini leo imekuwa tofauti kwa vijana hawa kupata fursa adhimu kama hiyo.

Ametoa wito kwa Watanzania wote kufika uwanja wa taifa kwa wingi  Mei 27, mwaka huu kushuhudua mashindano hayo ambapo hakuna kiingilio chochote na mgeni rasmi anatarajia kuwa ni Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa. Tembelea jambotz.co.tz kila siku upate habari moto moto. Tufollow Facebook, Instagram, YouTube na twitter @jambotz Continue reading

UTAFITI: WANAWAKE WA RWANDA NA KENYA KUISHI MIAKA MINGI

Related image

Wanawake nchini Rwanda na Kenya ndio wanaotarajiwa kuishi muda mrefu zaidi miongoni mwa wanawake na wanaume katika nchi za Afrika Mashariki, kwa mujibu wa takwimu. Umri wa wanawake kuishi Rwanda kwa sasa ni miaka 69.3 na nchini Kenya ni miaka 69.0.

Hata hivyo, umri wa kuishi wa wanaume Uganda ndio ulioongezeka zaidi katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita, ambapo umepanda kwa miaka 13.5.

Nchini Tanzania, umri wa kawaida wa kuishi kwa wanawake kufikia mwaka 2016 ulikuwa miaka 66, ongezeko la miaka 10 ukilinganisha na mwaka 1990 kwa mujibu wa Utafiti wa Mzigo wa Maradhi Duniani mwaka 2016, ulioratibiwa na Taasisi ya Takwimu za Afya na Utathmini. Continue reading

TMA YATOA TAHADHARI YA MVUA KUBWA ZAIDI INAYOKUJA

Kama ulidhani kwamba hekaheka zinazotokana na mvua inazoendelea kunyesha katika maeneo mengi ya nchi hususan mikoa ya Pwani inakaribia kumalizika, utakuwa unajidanganya.

Chukua tahadhari, tena kubwa kwani Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua hiyo haitegemewi kupungua katika siku za karibuni na angalizo kubwa zaidi ni kwamba kuna uwezekano kuongezeka maradufu ifikapo Mei 10 na kwamba inatarajiwa kuendelea kunyesha hadi mwishoni mwa mwezi huu.

“Zitaendelea kunyesha katika viwango tofauti kutokana na mambo mengi ikiwamo mabadiliko katika bahari na ndiyo maana kuna wakati unaweza ukaona kijua kidogo kisha mvua zinaendelea. Wananchi lazima wachukue tahadhari,” Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi alisema jana alipokuwa akizungumzia hali ya mvua zinazonyesha. Continue reading

LEMA AMSHANGAA GAMBO KUSEMA WAO NI MARAFIKI KANISANI

Image result for Lema gamboJana katika misa ya kumsimika Askofu mkuu wa jimbo Katoliki la Arusha, mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alipopewa nafasi ya kumkaribisha Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania alitumia nafasi hiyo pia kuwatambulisha baadhi ya viongozi wa serikali na wastaafu waliohudhulia misa hiyo takatifu.
Akimtambulisha Mbunge wa Arusha mjini  Gambo alisema “napenda pia kutambua uwepowa rafiki yangu mbunge wa Arusha Mjini Mh. Godbless Lema”. Katka pitapita zetu mtandaoni tukakutana na tweet ya Lema ikisema:-
“Katika Ibada ya kusimikwa Askofu, Rais aliongea neno la Mungu kuhusu Amani na Haki. Bila shaka demokrasia na haki vitashamiri tena. Askofu Amani yeye akasisitiza ushirikiano kisiasa bila kubaguana. Mrisho Gambo (RC) yeye akuogopa kuwa muongo madhabauni, eti aliniita Mimi rafiki yake.”

ROBOTS CAME TO TAKE AFRICAN JOBS

Within less than two decades it will be cheaper to operate robots in US factories than hire workers in Africa, a new report warns.

Falling automation costs are predicted to cause job losses as manufacturers return to richer economies.

Some analysts say poorer countries could be less impacted by this trend, however the Overseas Development Institute (ODI) suggests otherwise.

But its report adds African nations have time to prepare for the change.

“African countries must not shy away from manufacturing, but instead prepare by increasing access to internet, investing in technical skills and promoting technological innovation,” said Karishma Banga a senior research officer at ODI. Continue reading

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Powered by Live Score & Live Score App
403 Forbidden

403 Forbidden


nginx