Tag: Bongo Fleva

BABY J “KUOLEWA NA MTU MAARUFU ‘STRESS’ TUPU”

Image result for Jamila Abdallah ‘Baby J’Msanii wa Bongo Fleva kutoka Zanzibar, Jamila Abdallah ‘Baby J’, aliyewahi kutamba na ngoma za Bwashee Bwashee, Mpenzi Wangu pamoja na Moyo Wangu amesema kwamba kuolewa na mtu maarufu ni ‘stress’ kwani wengi huwa hawajatulia.

Baby J, ambaye anatarajia kuibuka na ujio mpya na mwanamuziki MwanaFA, aliongeza kuwa kwa upande wake ni vigumu kuolewa na staa kwa sababu amewahi kuwa kwenye uhusiano na staa ambaye hakupenda kumtaja jina na ameona ugumu wake.

“Kiukweli suala la kuolewa na staa kwa upande wangu ninaona kwamba ni stress tu, mastaa wengi hawajatulia. Nimekuwa kwenye uhusiano, ninafahamu kwa hiyo sidhani kama itatokea kuolewa na mtu maarufu!”

Tembelea jambotz.co.tz kila siku upate habari moto moto. Tufollow Facebook, Instagram, YouTube na twitter @jambotz

ALIKIBA AELEZA SABABU YA KUTOMPA KIGANJA DIAMOND

Image result for Alikiba na Diamond msibani

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba amefunguka kuhusu namna alivyosalimiana na msanii mwenzake, Nassib Abdul au Diamond kwa kumgeuzia mkono walipokutana katika msiba wa Masogange kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam.

Wawili hao walipokutana, Alikiba badala ya kumpa kiganja cha mkono kama ilivyozoeleka, alimpa mkono kwa kuugeuza jambo ambalo liliibua mjadala katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Akizungumza leo Ijumaa Mei 11, 2018 katika kipindi cha 360 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Clouds, ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipofunga ndoa Aprili 19, 2018, Alikiba amesema usalimiaji ule ndio wanaotumia wanaume kusalimiana na hakuna kitu kingine. Continue reading

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Powered by Live Score & Live Score App
403 Forbidden

403 Forbidden


nginx