Category: Udaku

BABU TALE AREJEA MTAANI BAADA YA KUSOTA RUMANDE KWA SIKU MBILI

Image result for Hamis TaletaleMkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection na Meneja wa Diamond Platnumz, Hamis Taletale maarufu Babutale ameachiwa kutoka Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam tangu jana Alhamisi na sasa yupo uraiani japo haijafahamika iwapo yupo nje kwa dhamana au vinginevyo.

Tale alifikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar, juzi Jumatano Mei 23, 2018 kufuatia kesi yake anayodaiwa na Sheikh Hashim Mbonde kiasi cha Tsh. Milioni 250 ambapo kesi hiyo iliahirishwa baada ya hakimu aliyetoa amri ya kumkamata kutokuwepo mahakamani hapo.

Kipindi cha nyuma mahakama hiyo ilimwamuru Babu Tale alipe Sh. milioni 250 Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde, baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.

Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa, Februari 18, mwaka juzi, katika kesi ya madai namba 185 ya mwaka 2013, iliyofunguliwa na Sheikh Mbonde aliyewalalamikia ndugu hao kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake. Tembelea jambotz.co.tz kila siku upate habari moto moto. Tufollow Facebook, Instagram, YouTube na twitter @jambotz

BABY J “KUOLEWA NA MTU MAARUFU ‘STRESS’ TUPU”

Image result for Jamila Abdallah ‘Baby J’Msanii wa Bongo Fleva kutoka Zanzibar, Jamila Abdallah ‘Baby J’, aliyewahi kutamba na ngoma za Bwashee Bwashee, Mpenzi Wangu pamoja na Moyo Wangu amesema kwamba kuolewa na mtu maarufu ni ‘stress’ kwani wengi huwa hawajatulia.

Baby J, ambaye anatarajia kuibuka na ujio mpya na mwanamuziki MwanaFA, aliongeza kuwa kwa upande wake ni vigumu kuolewa na staa kwa sababu amewahi kuwa kwenye uhusiano na staa ambaye hakupenda kumtaja jina na ameona ugumu wake.

“Kiukweli suala la kuolewa na staa kwa upande wangu ninaona kwamba ni stress tu, mastaa wengi hawajatulia. Nimekuwa kwenye uhusiano, ninafahamu kwa hiyo sidhani kama itatokea kuolewa na mtu maarufu!”

Tembelea jambotz.co.tz kila siku upate habari moto moto. Tufollow Facebook, Instagram, YouTube na twitter @jambotz

AUNT EZEKIEL AWAWAKIA WANAOMUITA MUMEWE DANSA

Image result for aunt ezekiel na mose iyoboStaa wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel ameibuka na kuwacharukia wale wanaomchukulia baba watoto wake, Mozes Iyobo kama dansa wakati yeye anamuona kama mkurugenzi

Aunt alisema amekuwa akifuatilia kwenye mitandao ya kijamii na kuona watu wakimchukulia poa Iyobo lakini anawaambia tu, yeye kwake anamuona kama mkurugenzi.

“Waache kumchukulia poa Moze wangu. Mimi namuona kama mkurugenzi fulani hivi, wao wakiona mtuanacheza muziki hawajui kama ni kazi, hawathamini na kuonesha dharau tu mitandaoni,” alisema Aunt.

STEVE NYERERE AMPA ‘MAKAVU’ MAMA KANUMBA

Muigizaji filamu za kibongo Steven Nyerere amefunguka juu ya kitendo cha Mama Kanumba kutoridhishwa na kubadilishiwa adhabu Elizabeth Michael (Lulu) ambaye alifungwa kwa kosa la kumuua bila kukusudia mwanaye Kanumba.

Akizunguma na mwandishi wa habari Steve Nyerere amesema kwamba amefuta namba ya mama Kanumba kwani hana shughuli naye, na asitake kushindana na serikali kwa sababu hata yeye ilimsaidia alipohitaji msaada.

“Mimi namba ya yule mama nimeifuta nimekasirika nimeona hana shughuli tu, kwa sababu anaongea vitu ambavyo havipo yaani, na sikioni kama kina tija, unajua kuna vitu vingine sio vya kukurupuka kuongea, unatakiwa ukae na watu wakupe hata ushauri, halafu yeye sio mtu wa kugombana na serikali, serikali alipokufa Kanumba Continue reading

ALIKIBA AELEZA SABABU YA KUTOMPA KIGANJA DIAMOND

Image result for Alikiba na Diamond msibani

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba amefunguka kuhusu namna alivyosalimiana na msanii mwenzake, Nassib Abdul au Diamond kwa kumgeuzia mkono walipokutana katika msiba wa Masogange kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam.

Wawili hao walipokutana, Alikiba badala ya kumpa kiganja cha mkono kama ilivyozoeleka, alimpa mkono kwa kuugeuza jambo ambalo liliibua mjadala katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Akizungumza leo Ijumaa Mei 11, 2018 katika kipindi cha 360 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Clouds, ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipofunga ndoa Aprili 19, 2018, Alikiba amesema usalimiaji ule ndio wanaotumia wanaume kusalimiana na hakuna kitu kingine. Continue reading

AJISALIMISHA POLISI BAADA YA MZIGO ALIOIBA KUNG’ANG’ANIA KICHWANI

 

Mkazi wa Mbezi, Dar es salaam, Frank Japhet (23) amelazimika kujisalimisha kituo cha polisi Mlandizi, Kibaha, Pwani, baada ya mzigo wa mahindi unaokadiriwa kuwa na uzito wa kg 20, anaodaiwa kuuiba kung’ang’ania kichwani.

Kwa maelezo ya mtuhumuwa huyo aliyoyatoa kituoni hapo, mzigo huo wa mahindi, uliofungwa kwenye kiroba aliuiba kwa mama mmoja eneo la mtaa wa Nyambwiro, Mlandizi, Kibaha, Pwani majira ya saa 7.00 usiku wa kuamkia leo.

Amesema, alipoondoka na mzigo huo hadi eneo la stendi ya Mlandizi alipokuwa auache kwa mwenzake ili arudie mzigo mwingine, mzigo huo uling’ang’ania kichwani. Continue reading

HARMONIZE AELEZA SABABU YA KUMCHUNIA ALIKIBA MSIBANI

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva kutoka label ya WCB, Harmonize amefunguka sababu ya kutompa mkono Alikiba walipokutana katika msiba wa Agness Gerald ‘Masogange’.

Muimbaji huyo anayefanya vizuri na ngoma ‘Kwa Ngwaru’ ameiambia The Playlist ya Times FM kuwa mambo yote yanayozungumzwa si ya kweli, bali walisalimiana ila si kwa kushikana mikono.

“Unajua asilimia kubwa ya watu wanaozungumza hawakuwa pale, unajua unapomzungumzia Alikiba ni mtu ambaye amefanya muziki wetu upate heshima kwa namna moja au nyingine, kama msanii namheshimu siwezi nikakutana na mtu halafu nisimsalimie, sio kweli,” amesema na kuongeza:

“Kilichofanyika ni kwamba Diamond kamsalimia kwa mkono, wamesamiliana kwa mkono. Mimi nimekuja nimezunguka nikaona kwa kuwa Diamond kamsalimia kwa mkono, kamgeuzia kiganja, mimi nikamsalimia kwa sauti tu, tukakaa pale tukaendelea.”

LEMA AMSHANGAA GAMBO KUSEMA WAO NI MARAFIKI KANISANI

Image result for Lema gamboJana katika misa ya kumsimika Askofu mkuu wa jimbo Katoliki la Arusha, mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alipopewa nafasi ya kumkaribisha Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania alitumia nafasi hiyo pia kuwatambulisha baadhi ya viongozi wa serikali na wastaafu waliohudhulia misa hiyo takatifu.
Akimtambulisha Mbunge wa Arusha mjini  Gambo alisema “napenda pia kutambua uwepowa rafiki yangu mbunge wa Arusha Mjini Mh. Godbless Lema”. Katka pitapita zetu mtandaoni tukakutana na tweet ya Lema ikisema:-
“Katika Ibada ya kusimikwa Askofu, Rais aliongea neno la Mungu kuhusu Amani na Haki. Bila shaka demokrasia na haki vitashamiri tena. Askofu Amani yeye akasisitiza ushirikiano kisiasa bila kubaguana. Mrisho Gambo (RC) yeye akuogopa kuwa muongo madhabauni, eti aliniita Mimi rafiki yake.”
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Powered by Live Score & Live Score App
403 Forbidden

403 Forbidden


nginx