Category: Habari za Kitaifa

MWIZI WA MAHINDI ALIEZUA GUMZO AFIKISHWA MAHAKAMANI

Mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam, Frank Joseph amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Mlandizi mkoani Pwani akishtakiwa kwa wizi wa mahindi.

Joseph ambaye tukio la kukamatwa kwake liliibua hisia na mijadala mitandaoni ikidaiwa alishindwa kutua mzigo aliodaiwa kuuiba, alisomewa shtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi, Nabwike Mbaba.

Mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya jinai namba 124/2018 akidaiwa kuiba mahindi debe moja yenye thamani ya Sh20,000. Baada ya kusomewa shtaka, mshtakiwa huyo alikiri kutenda kosa. Continue reading

TMA YATOA TAHADHARI YA MVUA KUBWA ZAIDI INAYOKUJA

Kama ulidhani kwamba hekaheka zinazotokana na mvua inazoendelea kunyesha katika maeneo mengi ya nchi hususan mikoa ya Pwani inakaribia kumalizika, utakuwa unajidanganya.

Chukua tahadhari, tena kubwa kwani Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua hiyo haitegemewi kupungua katika siku za karibuni na angalizo kubwa zaidi ni kwamba kuna uwezekano kuongezeka maradufu ifikapo Mei 10 na kwamba inatarajiwa kuendelea kunyesha hadi mwishoni mwa mwezi huu.

“Zitaendelea kunyesha katika viwango tofauti kutokana na mambo mengi ikiwamo mabadiliko katika bahari na ndiyo maana kuna wakati unaweza ukaona kijua kidogo kisha mvua zinaendelea. Wananchi lazima wachukue tahadhari,” Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi alisema jana alipokuwa akizungumzia hali ya mvua zinazonyesha. Continue reading

WATU SITA WAHIFIWA KUFA MAJI KISIWANI MAFIA, PWANI

Watu sita wanahofiwa kufa maji baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kupinduka bahari, karibu na Kisiwa cha Mafia mkoani Pwani, kutokana na dhoruba kali.

Mbunge wa jimbo la Mafia, mkoani Pwani Mbaraka Dau amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

“Mwishoni mwa wiki hii ilitokea ajali ya boti iliyosababisha watu sita, miongoni mwao raia sita wa Tanzania na mmoja mwenye asili ya Marekani, waliokuwa wakisafiri kutoka katika bandari ya Nyamisati iliyoko wilaya ya Kibiti mkoa wa Pwani, wakielekea katika pwani ya Kilindoni iliyoko katika wilaya ya Mafia katika shughuli za kimishionari (masuala ya dini ya Kikristo)”. Continue reading

WAZIRI ‘NONDO AKISHINDA KESI ATAREJESHWA CHUONI’

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amesimamishwa masomo ili kulindwa, asipoteza sifa za kuwa mwanafunzi wa chuo hicho.

Kusimamishwa chuo kwa Nondo, kuliibua mjadala mkali wakati wa kuijadili bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakidai hatua hiyo ni aibu kwa chuo hicho.

Akijibu hoja hiyo jana Mei 2, 2018 bungeni mjini Dodoma, Naibu Waziri wa wizara hiyo, William Ole Nasha amesema kwa kuwa Nondo ana kesi kama akishinda anarejea chuoni na sheria inamlinda badala ya kumminya asipoteze sifa.

 

MBUNGE ‘BWEGE’ ALIAMSHA BUNGENI, AUNGA MKONO NA WARAKA WA MAASKOFU

Image result for MBUNGE wa Kilwa Kusini, Said BungaraMbunge wa Kilwa Kusini, Said Bungara (CUF) maarufu kama ‘Bwege’, amesema hakubaliani na kipengele kilichopo kwenye hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kinachoeleza kuwa nchi yetu ina amani sana.

Bungara amesema hakubaliani na hilo kutokana na matukio mawili yaliyotokea jimboni kwake; tukio la msikiti kuvamiwa na mtu mmoja kupoteza maisha na mwingine kubaki na ulemavu wa macho, huku tukio lingine ni la vijana kuchukuliwa katika mazingira ya kutatanisha na watu wanaodaiwa kuwa ni polisi ambapo mpaka leo watu wawili hawajajulikana walipo.

“Kuna Noah nyeusi ilikuja Kilwa na kukamata vijana wawili, usiku wake wakakamatwa vijana tisa, hatukujua wamepelekwa wapi, tulifuatilia mpaka Kituo cha Polisi Kilwa Masoko wakasema kweli wapo wameshikiliwa, nikamwandikia barua Waziri wa Mambo ya Ndani (Mwigulu Nchemba), tisa kati yao waliachiwa, lakini wawili hawajarudi mpaka sasa na hatujui wako wapi. Nataka leo, waziri atupatie vijana wetu hao na ushahidi upo.

“Leo mnapotuambia nchi hii ina amani mimi siwaelewi, watu wamepigwa risasi msikitini, mmoja amekufa, mwingine ametobolewa jicho na mwingine kachomwa moto ndevu, hawa watu wapo na serikali haikutoa tamko lolote. Hii nchi imeharibika. Ninaunga mkono waraka wa maaskofu kwa sababu maneno ya maaskofu ni maneno ya Mungu, tunataka amani na utulivu,” amesema Bwege.

HUYU HAPA MWANAMKE WA KWANZA KUPATA DEGREE TANZANIA

Mama Kamm akitunukiwa Tuzo.

Dkt Maria Kamm ndiye  mwanamke wa kwanza wa Tanzania kupata Shahada ya kwanza (Degree) na leo ametunukiwa tuzo ya heshima katika tuzo za Malkia wa Nguvu zinazoandaliwa na Clouds Media.

Image result for Dkt Maria KammMama Kamm ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Weruweru iliyopo Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, akiwa kama Mzalendo wa kweli, ametumia maisha yake kwa kiasi kikubwa kuwashauri na kuwaelimisha vijana katika masuala mbalimbali ya Taifa.
Mbunge Mstaafu na aliyekuwa Mkuu wa Sekondari ya Weruweru, Dk Maria Kamm akimshangilia Rais Magufuli alipoongea na wananchi wa Karanga

Mbunge Mstaafu na aliyekuwa Mkuu wa Sekondari ya Weruweru, Dk Maria Kamm akisalimiana na Rais Magufuli aliposimamishwa kuongea na wananchi wa Karanga Continue reading

FUNNY: GERMANY’S BEST APRIL FOOLS’ JOKES FROM 2018, EXPLAINED

Three people laughing at a Laptop (Colourbox)1. Berlin neighborhood passes alcohol ban

The joke: The German daily newspaper Berliner Zeitung reported on Sunday that the Prenzlauer Berg district of Berlin would introduce a ban on the sale of alcohol between 10 p.m. and 5 a.m. in July. Locals had complained about late night binge drinking and the tram smelling of beer, according to the paper.

Why it’s funny: If any of Berlin’s districts were to introduce a alcohol ban, it would be Prenzlauer Berg. The neighborhood is considered to be affluent, cosmopolitan and family friendly — a far cry from the more bohemian districts Berlin is known for. But it didn’t introduce the ban. That makes the joke funny.

2. German Heimat minister wants to reintroduce brown bears

The joke: Germany’s last brown bear was killed around 200 years ago. German Interior and “Heimat” (roughly translated as “home”) Minister Horst Seehofer told German public broadcaster ARD on Sunday: “The brown bear belongs to Germany like the wolf, bison and moose. Continue reading

Powered by Live Score & Live Score App
403 Forbidden

403 Forbidden


nginx