Author: admin

NDEGE YA CUBA YAANGUKA MUDA MFUPI BAADA YA KUPAA

A file picture of a Cubana de Aviacion aircraftNdege ya kubeba abiria aina ya Boeing 737 ya shirika la ndege la taifa Cuba, Cubana de Aviacion, imeanguka na kulipuka karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jose Marti, Havana, vyombo vya habari Cuba vinasema.

Shirika la habari la Prensa Latina limesema ndege hiyo imeanguka jana mei 18, muda mfupi baada ya kupaa. Taarifa zinasema ndege hiyo ilikuwa imewabeba watu 104. Kufikia sasa, hakujatolewa taarifa kuhusu hatima yao.

Radio Habana Cuba imeripoti kwamba ilikuwa ndege ya safari za ndani ya nchi na ilikuwa safarini kutoka Havana kwenda Holguin, mashariki mwa taifa hilo. Continue reading

SHIRIKA LA AFYA DUNIANI YAELEZEA HALI YA EBOLA DRC

Health workers at Bikoro hospital in DR CongoShirika la afya duniani WHO linasema mlipuko wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo haujafika kiwango cha kutangazwa hali ya dharura inayozusha wasiwasi wa kimataifa.

Katika mkutano huko Geneva ulioitishwa kwa dharura kujadili Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo shirika hilo limesema mlipuko wa sasa haijafikia vigezo vya kutangazwa hali ya hatari na halikupendekeza vizuizi vyovyote vya usafiri wala biashara.

Kamati ya muongozo wa kimataifa ya shirika hilo hatahivyo imesema kuna haja ya kuwa na wasiwasi kutokana na aina ya mlipuko wa sasa wa cDRC. Continue reading

AUNT EZEKIEL AWAWAKIA WANAOMUITA MUMEWE DANSA

Image result for aunt ezekiel na mose iyoboStaa wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel ameibuka na kuwacharukia wale wanaomchukulia baba watoto wake, Mozes Iyobo kama dansa wakati yeye anamuona kama mkurugenzi

Aunt alisema amekuwa akifuatilia kwenye mitandao ya kijamii na kuona watu wakimchukulia poa Iyobo lakini anawaambia tu, yeye kwake anamuona kama mkurugenzi.

“Waache kumchukulia poa Moze wangu. Mimi namuona kama mkurugenzi fulani hivi, wao wakiona mtuanacheza muziki hawajui kama ni kazi, hawathamini na kuonesha dharau tu mitandaoni,” alisema Aunt.

MESSI ABEBA TUZO YA MCHEZAJI BORA MWEZI APRILI

Image result for Lionel Messi

Mshambuliaji wa Barcelona na Timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi ‘L0a Pulga’ ametangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya soka ya Hispania ‘La Liga’, kwa mwezi Aprili.

Messi ambaye anaongoza kwa mabao kwenye ligi hiyo msimu huu ametangazwa mshindi leo Mei 18, 2018 asubuhi na bodi ya La Liga.

Katika mwezi Aprili, Messi amecheza Mechi 4 na kufunga mabao 6 huku akipiga ‘hat-trick’ mbili dhidi ya Leganes na Deportivo La Coruna ambazo zilimfanya kuongeza idadi ya mabao akimwacha hasimu wake, nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo. Continue reading

STEVE NYERERE AMPA ‘MAKAVU’ MAMA KANUMBA

Muigizaji filamu za kibongo Steven Nyerere amefunguka juu ya kitendo cha Mama Kanumba kutoridhishwa na kubadilishiwa adhabu Elizabeth Michael (Lulu) ambaye alifungwa kwa kosa la kumuua bila kukusudia mwanaye Kanumba.

Akizunguma na mwandishi wa habari Steve Nyerere amesema kwamba amefuta namba ya mama Kanumba kwani hana shughuli naye, na asitake kushindana na serikali kwa sababu hata yeye ilimsaidia alipohitaji msaada.

“Mimi namba ya yule mama nimeifuta nimekasirika nimeona hana shughuli tu, kwa sababu anaongea vitu ambavyo havipo yaani, na sikioni kama kina tija, unajua kuna vitu vingine sio vya kukurupuka kuongea, unatakiwa ukae na watu wakupe hata ushauri, halafu yeye sio mtu wa kugombana na serikali, serikali alipokufa Kanumba Continue reading

UTAFITI: WANAWAKE WA RWANDA NA KENYA KUISHI MIAKA MINGI

Related image

Wanawake nchini Rwanda na Kenya ndio wanaotarajiwa kuishi muda mrefu zaidi miongoni mwa wanawake na wanaume katika nchi za Afrika Mashariki, kwa mujibu wa takwimu. Umri wa wanawake kuishi Rwanda kwa sasa ni miaka 69.3 na nchini Kenya ni miaka 69.0.

Hata hivyo, umri wa kuishi wa wanaume Uganda ndio ulioongezeka zaidi katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita, ambapo umepanda kwa miaka 13.5.

Nchini Tanzania, umri wa kawaida wa kuishi kwa wanawake kufikia mwaka 2016 ulikuwa miaka 66, ongezeko la miaka 10 ukilinganisha na mwaka 1990 kwa mujibu wa Utafiti wa Mzigo wa Maradhi Duniani mwaka 2016, ulioratibiwa na Taasisi ya Takwimu za Afya na Utathmini. Continue reading

PROF. JAY ATABIRI ‘SUGU’ KUWA RAIS WA TANZANIA

Image result for professor jay

Mbunge wa Mikumi (Chadema), Joseph Haule ‘Profesa J’ amempongeza mbunge mwenzake wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kwa kuhitimisha mafunzo ya kisiasa na kusema sasa Sugu, anasubiri kuwa Rais wa Tanzania.

Profesa J ametoa utabiri huo leo Mei 11, 2018 bungeni kabla ya kuanza kuchangia kwa bajeti ya wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji ya 2018/19, ameanza kwa kusema;

“Natoa pongezi kubwa sana kwa pacha wangu aka Sugu kwa kuhitimu mafunzo huko ndani ambayo yameongeza ujasiri na CV yake ya kisiasa na natumaini sasa hivi hatakuwa rais wa Mbeya bali anakwenda katika mchakato wa kuwa Rais wa Tanzania huko mbeleni.” Continue reading

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Powered by Live Score & Live Score App
403 Forbidden

403 Forbidden


nginx