Day: May 8, 2018

MBUNGE ‘BWEGE’ ATAKA SERIKALI IUZE NDEGE MOJA

Mbunge wa Kilwa Kusini, Suleiman Bungara (maarufu kama ‘Bwege’), ameitaka serikali kuuza moja ya ndege zake za Bombardier zilizonunuliwa ili kutatua tatizo la maji nchini.

Pia amemtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai kuongoza zoezi la kupiga kura ili wabunge waamue kipaumbele iwapo wanahitaji maji au ndege.

Bwege ametoa kauli hiyo leo wakati akichangija bajeti ya wizara ya maji na umwagiliaji ambapo pamoja na mambo mengine amesema tatizo si mawaziri mizigo bali ni serikali.

“Kama hakuna maji hadi 2020, CCM kwa heri kwa sababu magereza hakuna maji, lazima tutie udhu tupate maji naomba sana spika tuuze ndege tutatue tatizo la maji. Kwa kuwa uko vizuri leo piga kura wanaotaka ndege na maji tuone. Continue reading

MWIZI WA MAHINDI ALIEZUA GUMZO AFIKISHWA MAHAKAMANI

Mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam, Frank Joseph amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Mlandizi mkoani Pwani akishtakiwa kwa wizi wa mahindi.

Joseph ambaye tukio la kukamatwa kwake liliibua hisia na mijadala mitandaoni ikidaiwa alishindwa kutua mzigo aliodaiwa kuuiba, alisomewa shtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi, Nabwike Mbaba.

Mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya jinai namba 124/2018 akidaiwa kuiba mahindi debe moja yenye thamani ya Sh20,000. Baada ya kusomewa shtaka, mshtakiwa huyo alikiri kutenda kosa. Continue reading

MSUVA “NIMETUMIA SANA LUGHA YA ISHARA KUELEWANA NA WACHEZAJI WENZANGU”

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Taifa Stars, Saimon Msuva ametimiza miezi tisa sawa na siku siku 276 tangu ajiunge na Difaa El Jadida ya Morocco ambako amekuwa gumzo katika mitaa ya Jadida na Rabat.

Msuva anasema alijipanga na changamoto za Morocco hasa kwenye Lugha kutokana na asilimia kubwa ya wakazi wa nchi hiyo kuongea Kiarabu na Kifaransa.

“Nilijisema kuwa safari hii kazi ninayo maana sikuwa najua Kiarabu wala Kifaransa, Kiingereza kuna mazingira kilikuwa kinanisaidia lakini kiukweli nimetumia sana lugha ya ishara ili kuelewana na wachezaji wenzangu”. Continue reading

KOCHA MPYA WA ARSENAL KUJULIKANA HIVI KARIBUNI, WANAOTAJWA KUCHUKUA NAFASI HIYO HAWA HAPA

Klabu ya soka ya Arsenal ina uhakika wa kumtangaza meneja mpya wa timu hiyo atakayechukua mikoba ya Arsene Wenger, kabla ya kuanza kwa fainali za michuano ya kombe la dunia.

Washika mitutu hao wa London, hawajaweka hadharani lini itakuwa muda rasmi wa mwisho wa kusaka meneja mpya, lakini meneja mpya atajulikana kabla ya tarehe 14 Juni, tarehe ambayo michuano ya kombe la dunia itakuwa inaanza kutimua vumbi huko nchini Urusi.

Wenger aliyedumu katika klabu ya Arsenal kwa miaka 22, ataiongoza timu hiyo katika michezo miwili iliyosalia kabla ya kumalizika kwa ligi jumapili ya Mei 13. Continue reading

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Powered by Live Score & Live Score App
403 Forbidden

403 Forbidden


nginx