Day: May 6, 2018

TMA YATOA TAHADHARI YA MVUA KUBWA ZAIDI INAYOKUJA

Kama ulidhani kwamba hekaheka zinazotokana na mvua inazoendelea kunyesha katika maeneo mengi ya nchi hususan mikoa ya Pwani inakaribia kumalizika, utakuwa unajidanganya.

Chukua tahadhari, tena kubwa kwani Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua hiyo haitegemewi kupungua katika siku za karibuni na angalizo kubwa zaidi ni kwamba kuna uwezekano kuongezeka maradufu ifikapo Mei 10 na kwamba inatarajiwa kuendelea kunyesha hadi mwishoni mwa mwezi huu.

“Zitaendelea kunyesha katika viwango tofauti kutokana na mambo mengi ikiwamo mabadiliko katika bahari na ndiyo maana kuna wakati unaweza ukaona kijua kidogo kisha mvua zinaendelea. Wananchi lazima wachukue tahadhari,” Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi alisema jana alipokuwa akizungumzia hali ya mvua zinazonyesha. Continue reading

WATU SITA WAHIFIWA KUFA MAJI KISIWANI MAFIA, PWANI

Watu sita wanahofiwa kufa maji baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kupinduka bahari, karibu na Kisiwa cha Mafia mkoani Pwani, kutokana na dhoruba kali.

Mbunge wa jimbo la Mafia, mkoani Pwani Mbaraka Dau amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

“Mwishoni mwa wiki hii ilitokea ajali ya boti iliyosababisha watu sita, miongoni mwao raia sita wa Tanzania na mmoja mwenye asili ya Marekani, waliokuwa wakisafiri kutoka katika bandari ya Nyamisati iliyoko wilaya ya Kibiti mkoa wa Pwani, wakielekea katika pwani ya Kilindoni iliyoko katika wilaya ya Mafia katika shughuli za kimishionari (masuala ya dini ya Kikristo)”. Continue reading

Powered by Live Score & Live Score App
403 Forbidden

403 Forbidden


nginx