Day: May 3, 2018

AJISALIMISHA POLISI BAADA YA MZIGO ALIOIBA KUNG’ANG’ANIA KICHWANI

 

Mkazi wa Mbezi, Dar es salaam, Frank Japhet (23) amelazimika kujisalimisha kituo cha polisi Mlandizi, Kibaha, Pwani, baada ya mzigo wa mahindi unaokadiriwa kuwa na uzito wa kg 20, anaodaiwa kuuiba kung’ang’ania kichwani.

Kwa maelezo ya mtuhumuwa huyo aliyoyatoa kituoni hapo, mzigo huo wa mahindi, uliofungwa kwenye kiroba aliuiba kwa mama mmoja eneo la mtaa wa Nyambwiro, Mlandizi, Kibaha, Pwani majira ya saa 7.00 usiku wa kuamkia leo.

Amesema, alipoondoka na mzigo huo hadi eneo la stendi ya Mlandizi alipokuwa auache kwa mwenzake ili arudie mzigo mwingine, mzigo huo uling’ang’ania kichwani. Continue reading

WAZIRI ‘NONDO AKISHINDA KESI ATAREJESHWA CHUONI’

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amesimamishwa masomo ili kulindwa, asipoteza sifa za kuwa mwanafunzi wa chuo hicho.

Kusimamishwa chuo kwa Nondo, kuliibua mjadala mkali wakati wa kuijadili bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakidai hatua hiyo ni aibu kwa chuo hicho.

Akijibu hoja hiyo jana Mei 2, 2018 bungeni mjini Dodoma, Naibu Waziri wa wizara hiyo, William Ole Nasha amesema kwa kuwa Nondo ana kesi kama akishinda anarejea chuoni na sheria inamlinda badala ya kumminya asipoteze sifa.

 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Powered by Live Score & Live Score App
403 Forbidden

403 Forbidden


nginx