Day: May 2, 2018

HARMONIZE AELEZA SABABU YA KUMCHUNIA ALIKIBA MSIBANI

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva kutoka label ya WCB, Harmonize amefunguka sababu ya kutompa mkono Alikiba walipokutana katika msiba wa Agness Gerald ‘Masogange’.

Muimbaji huyo anayefanya vizuri na ngoma ‘Kwa Ngwaru’ ameiambia The Playlist ya Times FM kuwa mambo yote yanayozungumzwa si ya kweli, bali walisalimiana ila si kwa kushikana mikono.

“Unajua asilimia kubwa ya watu wanaozungumza hawakuwa pale, unajua unapomzungumzia Alikiba ni mtu ambaye amefanya muziki wetu upate heshima kwa namna moja au nyingine, kama msanii namheshimu siwezi nikakutana na mtu halafu nisimsalimie, sio kweli,” amesema na kuongeza:

“Kilichofanyika ni kwamba Diamond kamsalimia kwa mkono, wamesamiliana kwa mkono. Mimi nimekuja nimezunguka nikaona kwa kuwa Diamond kamsalimia kwa mkono, kamgeuzia kiganja, mimi nikamsalimia kwa sauti tu, tukakaa pale tukaendelea.”

FACEBOOK MBIONI KUANZISHA PROGRAM YA KUWAPATANISHA WAPENDANAO

Hivi karibuni kampuni hiyo ilikumbwa na kashfa ya kutothamini faragha za watumiaje wake huku watumiaji zaidi ya millioni hamsini walidukuliwa katika kipindi cha uchaguzi wa Marekani.

Kampuni ya facebook inaongeza faragha kwa watumiaji wake kwa kuweka sehemu ya kufuta historia ya ulichokitafuta katika mtandao huo wa kijamii.

Aidha amesema kwamba programu hiyo itaangazia uhusiano wa muda mrefu na sio urafiki wa muda mfupi na itawatenganisha marafiki na watu wanaotarajiwa kuwa na uhusiano.

”Programu hii itakuwa na kiwango cha juu cha siri na usalama kutoka mwanzo”, aliongeza.

 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Powered by Live Score & Live Score App
403 Forbidden

403 Forbidden


nginx