WAWILI KUIWAKILISHA TANZANIA KWENYE MASHINDANO YA KUHIFADHI QURAN

Mstahiki Meya  wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Chaulembo (kushoto) akikabidhi bendera ya Taifa ili kuiwakilisha nchi katika mashindano  ya 19 ya kusoma na kuhifadhi Quran tukufu Afrika.

Watanzania wawili wamekabidhiwa bendera ya Taifa ili kuiwakilisha nchi katika mashindano makubwa ya 19 ya kusoma na kuhifadhi Quran tukufu Afrika yatakayofanyika nchini.

Akikabidhi bendera hiyo Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Chaulembo, kwa wawakilishi pekee ambao ni Shujaa Sulemani kutoka Morogoro na Mbwana Dadi kutoka Pemba amesema kuwa, imezoeleka mara nyingi bendera yetu wanakabidhiwa timu za mpira, lakini leo imekuwa tofauti kwa vijana hawa kupata fursa adhimu kama hiyo.

Ametoa wito kwa Watanzania wote kufika uwanja wa taifa kwa wingi  Mei 27, mwaka huu kushuhudua mashindano hayo ambapo hakuna kiingilio chochote na mgeni rasmi anatarajia kuwa ni Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa. Tembelea jambotz.co.tz kila siku upate habari moto moto. Tufollow Facebook, Instagram, YouTube na twitter @jambotz Continue reading

BABU TALE AREJEA MTAANI BAADA YA KUSOTA RUMANDE KWA SIKU MBILI

Image result for Hamis TaletaleMkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection na Meneja wa Diamond Platnumz, Hamis Taletale maarufu Babutale ameachiwa kutoka Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam tangu jana Alhamisi na sasa yupo uraiani japo haijafahamika iwapo yupo nje kwa dhamana au vinginevyo.

Tale alifikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar, juzi Jumatano Mei 23, 2018 kufuatia kesi yake anayodaiwa na Sheikh Hashim Mbonde kiasi cha Tsh. Milioni 250 ambapo kesi hiyo iliahirishwa baada ya hakimu aliyetoa amri ya kumkamata kutokuwepo mahakamani hapo.

Kipindi cha nyuma mahakama hiyo ilimwamuru Babu Tale alipe Sh. milioni 250 Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde, baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.

Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa, Februari 18, mwaka juzi, katika kesi ya madai namba 185 ya mwaka 2013, iliyofunguliwa na Sheikh Mbonde aliyewalalamikia ndugu hao kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake. Tembelea jambotz.co.tz kila siku upate habari moto moto. Tufollow Facebook, Instagram, YouTube na twitter @jambotz

PICHA ZA MAALIM SEIF ALIVYOPOKELEWA NA MKUU WA MKOA WA MWANZA

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amepokea ugeni wa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) na Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hammad aliyefika Ofisini kwake akiwa ziara ya kikazi Mkoani humo jana Alhamisi, Mei 24, 2018.

Tembelea jambotz.co.tz kila siku upate habari moto moto. Tufollow Facebook, Instagram, YouTube na twitter @jambotz

KAULI YA KOREA KASKAZINI BAADA YA TRUMP KUFUTA MKUTANO WAO

Leo May 25, 2018 Serikali ya Korea Kaskazini imesema kwamba iko tayari kufanya mazungumzo na Washington wakati wowote kutatua matatizo kati yao, baada ya Marekani kuufutilia mbali mkutano wa kihistoria kati ya viongozi hao wawili.

Korea Kaskazini ilionyesha majuto juu ya uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump kusitisha mkutano huo ambao ulikuwa umepangwa kufanyika June 12, 2018 nchini Singapore, Waziri wa Kwanza wa Makamu wa Nje, Kim Kye Gwan alisema.

Siku ya Alhamisi Trump alimtumia Kim Jong Un barua ya kuufutilia mbali mkutano huo. Tembelea jambotz.co.tz kila siku upate habari moto moto. Tufollow Facebook, Instagram, YouTube na twitter @jambotz

KOCHA SIMBA ATIA NENO KUHUSU KUONDOKA KWA KICHUYA

Kocha Msaidizi wa Simba, Mrundi, Masoud Djuma, wakiwa wamebakiza mechi moja waweze kukamilisha msimu wa ligi kuu ameibuka na kusema kuwa wachezaji waliomaliza mkataba na mabingwa hao wasiondoke ili wacheze Klabu Bingwa msimu ujao.

Simba ambao ndiyo mabingwa wapya wa msimu wa 2017/18, walikabidhiwa kombe lao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, Jumamosi iliyopita ambapo itashiriki Klabu Bingwa Afrika msimu ujao.

Akizungumza na mwandishi wahabari hii, Djuma alisema kuwa wao wanauachia uongozi kuweza kushughulikia masuala ya mikataba ya wachezaji lakini pia hata wachezaji wenyewe kama wanataka kucheza ligi hiyo, basi waongeze mkataba mwingine katika klabu hiyo.

“Kuhusu wachezaji waliomaliza mikataba yao akiwemo Kichuya hilo tunawachia viongozi washughulikie na hata wachezaji wenyewe ndiyo wana maamuzi ya kubaki au kuondoka, ila wanajua kuwa msimu ujao tunacheza Klabu Bingwa Afrika hivyo ni fursa kwao kushiriki kama wakiondoka basi watakosa nafasi hii muhimu,” alisema Djuma.

Baadhi ya wachezaji ambao mikataba yao imemalizika ni Kichuya, Said Ndemla, Mzamiru Yassin na Laudit Mavugo. Tembelea jambotz.co.tz kila siku upate habari moto moto. Tufollow Facebook, Instagram, YouTube na twitter @jambotz

Na Champion

BABY J “KUOLEWA NA MTU MAARUFU ‘STRESS’ TUPU”

Image result for Jamila Abdallah ‘Baby J’Msanii wa Bongo Fleva kutoka Zanzibar, Jamila Abdallah ‘Baby J’, aliyewahi kutamba na ngoma za Bwashee Bwashee, Mpenzi Wangu pamoja na Moyo Wangu amesema kwamba kuolewa na mtu maarufu ni ‘stress’ kwani wengi huwa hawajatulia.

Baby J, ambaye anatarajia kuibuka na ujio mpya na mwanamuziki MwanaFA, aliongeza kuwa kwa upande wake ni vigumu kuolewa na staa kwa sababu amewahi kuwa kwenye uhusiano na staa ambaye hakupenda kumtaja jina na ameona ugumu wake.

“Kiukweli suala la kuolewa na staa kwa upande wangu ninaona kwamba ni stress tu, mastaa wengi hawajatulia. Nimekuwa kwenye uhusiano, ninafahamu kwa hiyo sidhani kama itatokea kuolewa na mtu maarufu!”

Tembelea jambotz.co.tz kila siku upate habari moto moto. Tufollow Facebook, Instagram, YouTube na twitter @jambotz

SUGU KUPELEKA SIRI NZITO ZA MAGEREZA BUNGENI

Image result for sugu bungeniMbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ leo atatua bungeni jijini Dodoma kuungana na wabunge wenzake wanaoendelea na vikao vya Bunge la Bajeti baada ya kurejea uraiani akitokea Gereza Kuu la Ruanda alikokuwa akitumikia kifungo.

Sugu na mwenzake, Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga walihukumiwa kifungo cha miezi mitano jela katika Mahakama ya Hakimu Mkazi-Mbeya Februari 26, baada ya kupatikana na hatia ya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli waliyoitoa Desemba 30, mwaka jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Sugu anasema akiwa bungeni, atawasilisha masikitiko yake juu ya maisha duni ya wafungwa gerezani ikiwamo malazi, mavazi, chakula na matibabu. Tembelea jambotz.co.tz kila siku upate habari moto moto. Tufollow Facebook, Instagram, YouTube na twitter @jambotz Continue reading

OKWI ‘KASEJA ALIFANYA NIJISIKIE VIBAYA’

Image result for Emmanuel Okwi KASEJAMshambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi, amesema kuwa licha ya timu hiyo kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara, kamwe hawezi kumsahau kipa wa Kagera Sugar, Juma Kaseja kwa kitendo chake alichomfanyia juzi Jumamosi katika Uwanja wa Taifa, Dar.

Juzi Jumamosi, Kaseja alidaka penalti ya Okwi katika mchezo wa Ligi Kuu Bara na kuiwezesha timu yake ya Kagera Sugar kuvunja rekodi ya Simba ambayo ilikuwa ikiishikilia ya kutofun­gwa katika ligi hiyo msimu huu.Image result for Emmanuel Okwi KASEJAKatika mchezo huo ambao ulikuwa ni wa mwisho wa Simba katika uwanja wake wa nyumbani na ambao pia ulishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli, Simba ilifungwa bao 1-0. Tembelea jambotz.co.tz kila siku upate habari moto moto. Tufollow Facebook, Instagram, YouTube na twitter @jambotz Continue reading

MWANAFUNZI AFARIKI BAADA YA KULIPUKIWA NA BETRI YA SIMU

Mwanafunzi wa darasa la nne wa shule ya msingi Sabasaba jijini Mwanza, Dotto Baraka (13) amefariki dunia baada ya kulipukiwa na betri ya simu aliyokuwa akiiunganisha na radio chakavu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana Mei 18, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema tukio hilo limetokea Mei 17 mtaa wa Igoma Mashariki jijini Mwanza.

“Baada ya kutoka shuleni, marehemu akiwa na watoto wenzake alianza kutengeneza radio chakavu kwa kuchukua betri ya simu na kuunganisha kwenye nyanya za radio hiyo akitumia mdomo ndipo mlipuko ulipotokea na kusababisha kifo chake,” amesema Kamanda Msangi. Continue reading

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Powered by Live Score & Live Score App
403 Forbidden

403 Forbidden


nginx